China yatoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuhimiza maendeleo yenye ubora
2023-03-30 18:12:12| cri

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Balozi Chen Xu, ametoa hotuba ya pamoja kwenye mkutano wa 52 wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kwa niaba ya nchi takriban 80 ikiwa ni pamoja na Brazil na Afrika Kusini juu ya kuadhimisha miaka 30 tangu ilipopitishwa “Taarifa ya Vienna na Mpango wa Utekelezaji”, na kutoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kusisitiza tena moyo wa taarifa hiyo na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu.

Hotuba hiyo ya pamoja imesema “Taarifa ya Vienna na Mpango wa Utekelezaji” ni mnara kwenye historia ya haki za binadamu duniani, na kusisitiza kuyaunganisha mambo mbalimbali kwenye shughuli za haki za binadamu, kutilia maanani maendeleo, na kuendeleza mawasiliano na ushirikiano.

Hotuba pia inasema nchi mbalimbali zinapaswa kutoa ahadi ya pamoja, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kuhimiza na kulinda haki zote za binadamu, na kuingiza nguvu zaidi chanya katika maendeleo ya mambo ya haki za binadamu duniani.