Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema, serikali ya nchi hiyo inachukua hatua mbalimbali ili kukabiliana kwa amani na wasiwasi wa usalama na amani ndani na nje ya nchi hiyo.
Abiy amesema hayo wakati akiwakilisha ripoti ya utendaji wa serikali kwa miezi sita katika Bunge la chini la nchi hiyo, iliyohusu amani na usalama, na masuala ya uchumi na jamii.
Akijibu maswali ya wabunge kuhusu masuala ya amani na usalama katika maeneo ya mpaka wa Ethiopia na Sudan na Sudan Kusini, waziri mkuu huyo amesema serikali yake inafanya kazi kwa karibu na serikali za nchi hizo mbili ili kukabiliana na masuala ya mpakani kwa njia ya mazungumzo.
Kuhusu hali ya usalama na amani nchini Ethiopia, Bw. Ahmed amesisitiza utayari na ahadi ya serikali yake kukabiliana na matishio yaliyopo kwa njia ya amani kupitia mazungumzo.