Makamu mkurugenzi mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Raia na Misaada ya Kibinadamu katika Umoja wa Ulaya Michael Kohler amesema, serikali ya Sudan Kusini inapaswa kurejesha amani na usalama ili iweze kupata msaada muhimu wa kifedha kutoka jamii ya kimataifa kwa mwaka huu na kuendelea.
Akizungumza mjini Juba, baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini Sudan Kusini, Koehler amesema kuendelea kwa mapigano ya kikabila na mashambulio dhidi ya wafanyakazi wa misaada na misafara yao kumezuia upatikanaji wa msaada wa kifedha unaohitajika zaidi nchini humo.
Mwaka jana, mashirika ya Umoja wa Mataifa yalizindua kampenzi ya mwaka 2023 ya kukabiliana na changamoto mbalimbali nchini Sudan Kusini, yakihitaji dola za kimarekani bilioni 1.7, lakini ni dola milioni 488.6 ndizo zimepatikana mpaka sasa.