Mawaziri wakuu wa China na Cote d’Ivoire wakutana
2023-03-30 08:44:43| CRI

Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na mwenzake wa Cote d’Ivoire Patrick Achi anayehudhuria Mkutano wa mwaka 2023 wa Baraza la Asia la Bo’ao unaofanyika mkoani Hainan, China. 

Bw. Li amesema, katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na uongozi wa rais wa China Xi Jinping na rais Alassane Ouattara wa Cote d’Ivoire, uhusiano kati ya pande hizo mbili umepata maendeleo kwa kasi katika pande zote. Pia ameeleza kuwa China inasifu Cote d’Ivoire kuunga mkono ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na mapendekezo ya maendeleo na usalama wa dunia, na kushikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja. Amesisitiza kuwa China itaendelea kuunga mkono kithabiti Cote d’Ivoire kuchukua njia ya kupata maendeleo ya mambo ya kisasa kwa kufuata hali yake yenyewe, na kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali.

Bw. Achi amesema Cote d’Ivoire itafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, kushiriki kikamilifu ushirikiano wa ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kupenda kuchukua fursa ya Maadhimisho ya Miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati yake na China, kukuza ushirikiano katika uwekezaji, kilimo, elimu na vijana, ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na mchakato wa utandawazi wa viwanda nchini humo.