China yaitaka jumuiya ya kimataifa izisaidie nchi za Afrika kuondoa matishio ya kigaidi
2023-03-30 08:31:55| cri


 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limefanya mkutano kuhusu ushirikiano na mashirika ya kikanda katika kupambana na ugaidi, ambapo mjumbe maalumu wa China kwenye masuala ya Afrika Bw. Liu Yuxi ameitaka jumuiya ya kimataifa izisaidie nchi za Afrika kuondoa  matishio ya kigaidi.

Amesema China inaitaka jumuiya ya kimataifa ifikie maoni ya pamoja kuhusu kupambana na ugaidi, kuongeza uwezo wa Afrika wa kulinda amani, kuondoa mazingira yanayofaa kwa ugaidi, na kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na mashirika yakikanda barani Afrika katika mapambano dhidi ya ugaidi.