China na Tanzania zaendelea kushirikiana kwenye sekta ya michezo
2023-03-30 22:53:21| cri

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Balozi Dk Pindi Chana ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika uendelezaji wa sekta ya michezo. Dk Chana amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Suo Peng, akieleza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika kubadilishana uzoefu wa wataalam wanaoweza kutoa ujuzi kwenye sekta hizo.

Amesema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano katika masuala mbalimbali tangu uhuru, ambapo viongozi waasisi wa pande mbili yaani Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong wa China walipoanzisha ushirikiano huo.

Dk. Chana amesema Tanzania na China zimeshaingia na kusaini makubaliano ya uendelezaji wa masuala mbalimbali ambayo pia Marais wa nchi hizo wamekuwa wakiyaeleza, hivyo ni wakati muafaka wa kuendelea kuyatekeleza.