Waziri wa mambo ya nje wa Honduras afanya mahojiano na CGTN
2023-03-30 13:41:32| cri

Waziri wa mambo ya nje wa Honduras Bw. Eduardo Enrique Reina amefanya mahojiano na Televisheni ya China CGTN mjini Beijing, na kusema kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Honduras na China kunaendana na wakati, na pia ni matarajio ya watu wao na kusisitiza tena kuwa Honduras inaunga mkono kithabiti kanuni ya China moja.

Bw. Reina amesema ziara yake nchini China imetimiza nia ya rais Xiomara Castro ya kutafuta uhusiano wa wazi zaidi wa kimataifa na kushiriki zaidi kwenye maendeleo ya dunia yenye ncha nyingi. Amesema China imefanya kazi muhimu sana katika kuhimiza uhusiano wa pande nyingi, na kuimarisha uhusiano na China kuna manufaa mengi.

Inatarajiwa kuwa ziara ya Rais Xiomara Castro nchini China inaweza kufanyika haraka iwezekanavyo. Pia anatarajia kuwezesha kundi la wafanyabiashara wa Honduras wazuru China katika wakati mwafaka ili pande hizo mbili zifahamishana zaidi katika sekta ya biashara.