Mtoto mwenye umri wa miaka 11 atoa mchango kwa ajili ya wakulima wa Botswana
2023-03-30 10:01:37| CRI

Ni wakati mwingine tena tunapokutana katika kipindi hiki cha DARAJA kinachokujia kila jumapili kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo tutakuwa na ripoti inayohusu mtoto mwenye umri wa miaka 11 anavyotoa mchango kwa ajili ya wakulima wa Botswana. Pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi yaliyoandaliwa na Tom Wanjala kuhusu Wachina wanavyomiminika kwa wingi nchini Kenya kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini humo.