Rais Xi asisitiza kuendelea kuimarisha juhudi za kujifunza na kutekeleza Fikra ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika zama mpya
2023-03-31 15:46:31| cri

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC ilikutana jana Machi 30 kwenye semina ya nne kuhusu kujifunza na kutekeleza Fikra ya Xi Jinping ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika zama mpya.

Kwenye semina hiyo Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Bw. Xi Jinping amesisitiza kuwa lengo la kuandaa semina hiyo ni kutoa mfano wa kuigwa, ili kusukuma mbele Chama kizima kuendeleza juhudi za kujifunza na kutekeleza Fikra ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika zama mpya, na hivyo kuimarisha msingi wa kinadharia na kifikra.

Bw. Xi amebainisha kuwa kujifunza na kutekeleza Fikra ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika zama mpya, ni matakwa ya kimsingi ya kufungua ukurasa mpya wa maendeleo kwenye safari mpya katika zama mpya. Amesisitiza kuwa kushikilia kuzatiti Chama kizima kwa matokeo mapya ya Umarx wenye umaalumu wa China na yanayoendana na zama zetu na kuyatumia kwenye utendaji wa kazi, ni uzoefu muhimu wa Chama kuweza kuweka historia na kutimiza ustawi.