Taasisi ya Elimu Tanzania kushirikiana na China ufundishaji wa somo la hisabati
2023-03-31 19:04:11| cri

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imeingia makubaliano ya miaka mitatu na Chuo Kikuu cha Shanghai cha nchini China ili kuboresha ufundishaji wa somo la hisabati ikiwemo mbinu wanazotumia kwa walimu pamoja na kufanya utafiti.

Mkurugenzi Mkuu TET Dkt. Aneth Komba amesema makubaliano hayo ya utafiti yatalenga kwenye somo la hisabati kutokana na changamoto za somo hilo kutofanya vizuri kwa kipindi kirefu, na ni suluhu nzuri kwa kuwa Shanghai ndiyo inaongoza kwa kutoa walimu na wanafunzi bora wa somo la hisabati duniani.

Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala wa TET Dkt Fika Mwakabungu amesema mradi huo utatoa motisha kwa walimu kutokana na kupewa njia sahihi za kuwafundisha wanafunzi wa Tanzania.

Amesema utafiti walioufanya umeonesha kuwa wataalam wa Shanghai wako mbele sana kwenye masuala ya ufundishaji wa somo la Hisabati.