Shirikisho la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema nchi za Afrika zinapaswa kutunga sera na kanuni za kisheria zinazowezesha safari za kuvuka mipaka kwa nguvukazi yenye ujuzi ili kutimiza ukuaji wa kiuchumi, utulivu na mshikamano.
Mkurugenzi wa Ofisi ya IOM kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Mohammed Abdiker amesema, kuondoa vikwazo kwa safari za ndani ya Afrika kwa watu wenye ujuzi kunapaswa kutoa ishara ya juhudi za baadaye za kutimiza matunda ya juhudi zinazoendelea za maingiliano ya bara hilo na kukabiliana na umasikini na majanga mengine ya kijamii.
Amesema, kutunga sheria rafiki za uhamiaji pia kutasaidia nchi za Afrika kufaidika kiuchumi na kijamii kutokana na uhuru wa kuvuka mipaka kwa wataalamu wa sekta mbalimbali.