Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya kivuko nchini Philippines yafikia 29
2023-03-31 08:36:59| cri


 

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya moto katika kivuko kwenye bahari karibu na Mkoa wa Basilan kusini nchini Philippines, imezidi 29.

Kikosi cha Ulinzi wa Pwani nchini humo kimesema, watu 230 waliokuwa kwenye kivuko hicho wameokolewa. Wafanyakazi wa utafutaji na uokoaji walipata miili 18 kwenye kivuko, na watu wengine 11 walikufa maji walipojirusha baharini kukwepa moto huo.