Wawekezaji wa Afrika Kusini kuangalia uwezekano wa kuwekeza nchini Tanzania
2023-03-31 22:03:30| cri

Ujumbe wa wafanyabiashara wasiopungua 30 kutoka Afrika Kusini umetembelea Tanzania kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya madini. Hatua hii inafuatia ziara ya hivi karibuni ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Afrika Kusini.

Kamishna wa Madini wa Tanzania Bw. Abdulrahman Mwanga, amesema Rais Samia alipotembelea Afrika Kusini wiki chache zilizopita, masuala mbalimbali yalijadiliwa na nchi mbili ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji nchini Tanzania.

Bw. Mwanga amesema ujio huo unaashiria kuwa sekta ya madini ina uwezekano wa kukua zaidi, ina fursa mbalimbali za uwekezaji; na hivyo basi ni muhimu hata kwa wawekezaji wa ndani kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta hiyo.