Afrika yajitahidi kutumia sarafu za nchi za Afrika katika biashara ya ndani ya bara hilo
2023-03-31 08:39:23| CRI

Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) linajitahidi katika matumizi ya sarafu za ndani katika biashara kati ya nchi za bara hilo.

Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya AfCFTA, Wamkele Mene amesema, biashara ya kuvuka mpaka kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) tayari inaendelea kupitia matumizi ya sarafu za nchi hizo badala ya kutumia dola ya kimarekani.

Amesema gharama ya kubadilisha sarafu kutokana na matumizi ya dola ya kimarekani katika biashara kati ya nchi za Afrika ni karibu na dola za kimarekani bilioni 5 kwa mwaka, na kuongeza kuwa, ili kuepuka gharama hiyo, Sekretarieti yake imeunda mfumo wa malipo na makubaliano kwa nchi za Afrika unaowezesha kufanya biashara kwa kutumia sarafu za nchi husika.