Jopo kuu la mahakama ya Manhattan mjini New York laamua kumfungulia mashtaka Donald Trump
2023-03-31 18:01:42| cri

Habari kutoka gazeti la “The New York Times” limesema jopo kuu la mahakama ya wilaya ya Manhattan katika jimbo la New York, Marekani limepiga kura na kuamua kumfungulia mashtaka rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kwa tuhuma za kumpatia mlungula nyota wa filamu za ngono Stormy Daniels ili kuficha siri ya mahusiano na Trump, pamoja na kughushi taarifa za biashara wakati aliposhiriki kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2016. Tuhuma kamili zitatangazwa katika siku za baadaye. Bw. Trump anakuwa rais wa kwanza wa zamani wa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya jinai.