Vyama vya Sudan vyaahirisha kusaini makubaliano ya mwisho ya kisiasa hadi Aprili 6
2023-04-03 21:49:48| cri

Vyama vya Sudan vinavyohusika katika mchakato wa kisiasa siku ya Jumamosi vilikubali kuahirisha utiaji saini wa makubaliano ya mwisho hadi Aprili 6.

Uamuzi huo ulitolewa wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu siku ya Jumamosi ambacho kiliwakutanisha Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sudan na Kamanda wa jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Utawala na Kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka Mohamed Hamdan Dagalo, viongozi wa vikosi vya kiraia, na wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali.

Makubaliano ya mwisho ya kisiasa, ambayo yanalenga kuunda mamlaka ya mpito ya kiraia nchini Sudan, yalipangwa kusainiwa Jumamosi, lakini tofauti kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka juu ya kifungu cha mageuzi ya usalama na kijeshi na ujumuishaji wa vikosi visivyo vya kawaida jeshini zimepelekea kuahirisha utiaji saini wa makubaliano hayo.