Mwanariadha mkenya Philimon Kiptoo Kipchumba alitwaa ubingwa wa Mashindano ya Mbio za Marathon ya Mwaka 2023 kwa wanaume yaliyofanyika Jumapili, huku Meseret Abebayehu Alemu kutoka Ethiopia akitwaa medali ya dhahabu ya mashindano hayo kwa wanawake.
Kipchumba amesema hii ni mara yake ya kwanza kushiriki Mashindano ya Mbio za Marathon za Xiamen, na kwamba mashindano hayo yalimvutia kutokana na idadi kubwa ya wanariadha na watazamaji wenye shauku kubwa.
Lencho Tesfaye Anbesa kutoka Ethiopia na Omar Ait Chitachen kutoka Morocco walitwaa medali za fedha na shaba kwa kutumia muda wa saa 2:08:29 na 2:08:59.
Ubingwa wa wanawake ulinyakuliwa na Alemu kutoka Ethiopia kwa kutumia saa 2:24:42, huku Gladys Chesir Kiptagelai kutoka Kenya akishika nafasi ya pili kwa kutumia saa 2:25:51, na mwenzake Guteni Shone Imana ambaye pia anatoka Ethiopia, alitwaa medali ya shaba akitumia muda wa saa 2:25:58.