Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.0 laikumba Papua New Guinea
2023-04-03 09:14:42| CRI

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 katika kipimo cha Richter limetokea leo nchini Papua New Guinea, lakini hadi sasa hakuna ripoti za vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani (USGS), tetemeko hilo lilitokea afajiri ya leo tarehe 3 Aprili.

Kituo cha Tahadhari za Tsunami cha Pasifiki (PTWC) hakikutoa onyo la tsunami kufuatia tetemeko hilo.

Papua New Guinea iliyoko kwenye makutano ya mabamba ya mabara, iko katika ukanda wa volkeno wa mzunguko wa Bahari ya Pasifiki, na inakumbwa na matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara.