Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kimeadhimisha mwaka wa uwepo wake nchini Somalia, kwa kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano ili kuimarisha amani na utulivu nchini humo.
Mjumbe maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) nchini Somalia na mkuu wa ATMIS Bw. Mohammed El-Amine Souef, amesema mapitio ya hali katika Maeneo ya Uwajibikaji ya ATMIS katika mwaka uliopita, yanaonesha kupungua kwa shughuli za kundi la al-Shabab, na hali ya usalama kote nchini Somalia ikiendelea kuwa shwari.
Hata hivyo amesema bado kuna changamoto katika baadhi ya maeneo, kwani kundi la Al-shabaab linaendesha mapambano yasio na usawa kwa kuwalenga raia wa kawaida.