Tume ya Umoja wa Afrika imewapongeza wafanyakazi wa China ikitambua “ushirikiano wao wa hali ya juu na wa kitaaluma” kwenye ujenzi wa mradi wa makao makuu ya Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Maradhi cha Afrika Africa CDC uliofadhiliwa na China.
Tume hiyo imezipongeza timu za uhandisi, ufundi na ugavi za China kwenye sherehe iliyofanyika kwenye makao makuu ya Africa CDC mjini Addis Ababa.
Akitoa pongezi hizo, kaimu mkurugenzi anayeshughulikia Maendeleo ya Kijamii, Utamaduni na Michezo wa tume hiyo Bibi Angela Martins, amesema wanaishukuru serikali ya China kwa kujenga kituo hicho muhimu, ambacho kimekuwa alama nyingine ya urafiki kati ya Afrika na China.