Washauri wawili wa kijeshi wa Iran wauawa katika mashambulizi ya anga lililofanywa na Israel dhidi ya Syria
2023-04-03 08:58:32| CRI

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran limesema mshauri mmoja wa kijeshi wa Iran ameuawa hivi karibuni katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel dhidi ya Syria, kufuatia kifo cha mshauri mwingine wa Iran kilichothibitishwa hapo awali, na kusema Iran italipiza kisasi kwa Israel kufuatia vifo cha washauri hao wawili.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Nasser Kanani, imesema mashambulizi ya mfululizo yaliyofanywa na Israel dhidi ya Syria yamekiuka mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya Syria na pia yamekiuka sheria za kimataifa, na kwamba damu ya washauri hao wawili wa Iran “haitamwagika bure.”

Amesema Iran itachukua hatua dhidi ya“vitendo hivyo vya uvamizi na jinai” katika pande za siasa na sheria, na kubaki na haki yake ya kuchukua hatua katika wakati mwafaka na mahali mwafaka.