Rais Xi ajibu barua ya wasanii mashuhuri wa kiarabu
2023-04-04 08:10:19| CRI

Rais Xi Jinping wa China amejibu barua aliyoandikiwa na wajumbe wa wasanii mashuhuri wa kiarabu walioshiriki kwenye ziara ya “Wasanii wa Njia ya Hariri” nchini China, akiwahamasisha kutengeneza zaidi kazi za usanii zinazoakisi urafiki kati ya China na nchi za kiarabu na kutoa michango mipya katika kuimarisha urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili.

Kwenye barua yake, Rais Xi amesema utamaduni unaweza kuunganisha mioyo, na sanaa inaweza kuunganisha dunia, na kwamba tangu kufunguliwa kwa Njia ya Hariri ya kale hadi ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, mawasiliano kati ya staarabu za China na za waarabu yamevuka maelfu ya miaka kwa kutambuana na kuheshimiana, na kuweka urithi wa kihistoria wa kufundishana.