Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mkurugenzi mkuu wa IOM
2023-04-04 09:53:23| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang amekutana na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM Bw. Antonio Vitorino hapa Beijing, na kutoa mwito kuimarisha ushirikiano katika siku za baadaye.

Bw. Qin amepongeza kazi ya Bw. Vitorino tangu aingie madarakani, huku akisema ni lazima kuboresha usimamizi wa uhamiaji wa kimataifa. Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kulinda haki halali na maslahi ya wahamiaji, kuwa na mtazamo wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kuwachukulia wahamiaji kwa msimamo wenye usawa, huku ikitakiwa kupinga uchochezi wa ubaguzi wa rangi na chuki za kikabila.

Bw. Qin amesema Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, kuimarisha mazungumzo, kuunga mkono mashirika ya uhamiaji katika kutoa mchango katika usimamizi wa uhamiaji wa kimataifa, huku ikitekeleza makubaliano ya kimataifa ya uhamiaji na kuhimiza mizunguko ya kawaida ya uhamiaji yenye usalama na utaratibu.