China yatoa ripoti ya miaka kumi tangu kutolewa pendekezo la kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja
2023-04-05 11:05:58| CRI

Mwaka 2023 ni mwaka wa kumi tangu kiongozi mkuu wa China Xi Jinping atoe dhana ya kujenga "Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja". Tarehe 4 Aprili, Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Fedha ya Chongyang ya Chuo Kikuu cha Renmin cha China ilitoa ripoti maalum ya "Maadhimisho ya Miaka 10 ya Kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja: Dhana Inayokuzwa Zaidi, Utekelezaji wa Kivitendo na Matarajio ya Baadaye" hapa Beijing. Hii ni ripoti ya kwanza ya washauri bingwa ndani na nje ya nchi ya kufanya majumuisho kuhusu utekelezaji wa kivitendo na maendeleo ya Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja katika miaka kumi iliyopita.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika miaka kumi iliyopita, Xi Jinping ametaja "jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja" katika angalau hotuba 670 muhimu, makongamano, shughuli, ukaguzi, mikutano, ziara nje ya nchi na salamu. Dhana hii ndiyo msingi wa kinadharia na kivitendo wa fikra za diplomasia za Xi Jinping, na pia ni "ndoto ya dunia" ya China iliyojengwa kwa kukamilisha dhana ya utaratibu wa dunia.