Rwanda na Kenya zimesaini makubaliano 10 yanayolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu, TEHAMA, afya, maendeleo ya watoto na kijinsia, maendeleo ya vijana na mengine.
Rais Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Kenya William Ruto wamesema kwenye mkutano wa pamoja na wanahabari mjini Kigali, kuwa nchi zao zimekubaliana kushirikiana kwa maslahi ya watu.
Rais Kagame amesema katika miaka kadhaa iliyopita, Rwanda na Kenya zimejenga uhusiano imara, na ushirikiano katika maeneo hayo mapya utazileta nchi hizo karibu zaidi.
Rais Ruto amesema makubaliano yaliyosainiwa kuhusu ushirikiano katika sekta mbalimbali yataimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kutia nguvu mpya na kuleta msukumo mpya kwa ukuaji wa uhusiano kati ya pande mbili.