Finland yajiunga rasmi na NATO
2023-04-05 09:01:31| CRI

Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi (NATO) jana Aprili 4 ilifanya sherehe ya kuikaribisha Finland kujiunga nayo kwenye makao makuu yake mjini Brussles. Finland imekuwa nchi mwanachama wa 31 wa NATO.

Mapema siku hiyo waziri wa mambo ya nje wa Finland Bw. Haavisto alikabidhi hati za Finland kujiunga na NATO kwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Anthony Blinken ambayo ni nchi inayohifadhi nyaraka za NATO.  

Wizara ya mambo ya nje ya Russia imetoa taarifa ikisema Ulaya ya Kaskazini lilikuwa moja ya maeneo yenye utulivu zaidi duniani, lakini baada ya Finland kujiunga na NATO, hali katika eneo hilo imekuwa na mabadiliko ya kimsingi, na kumekuwa na athari hasi kwa uhusiano kati ya Russia na Finland.