Rais Xi ahimiza juhudi zaidi za kupanda miti kwa ajili ya maendeleo ya kijani
2023-04-05 08:36:24| CRI

Rais Xi Jinping wa China ameshiriki kwenye shughuli ya upandaji miti mjini Beijing na kutoa wito wa juhudi kubwa zaidi za kupanda miti ili kuandika ukurasa mpya katika kuijenga China iliyo bora zaidi.

Rais Xi alitoa kauli hiyo alipohudhuria shughuli ya upandaji miti, shughuli ambayo anashiriki kwa mwaka wa 11 mfululizo akiwa Katibu Mkuu wa CPC.

Rais Xi amesema ushiriki wa viongozi kwenye upandaji miti utahamasisha wananchi kote nchini kufanya kazi kwa ajili ya ujenzi wa China iliyo bora zaidi.