Mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia na Iran wakutana hapa Beijing
2023-04-06 18:29:48| cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema kutokana na mapendekezo ya Saudi Arabia na Iran, China imewapokea mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia na Iran ambao wanakutana hapa Beijing. Hafla ya kusaini makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kibalozi kati ya Saudi Arabia na Iran imefanyika. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang amesema kuwa China inakaribisha na kupongeza jitihada za Saudi Arabia na Iran katika kuboresha uhusiano kati ya nchi mbili. China inapenda kuendelea kufanya kazi ya uratibu, kuziunga mkono pande hizo mbili kujenga uaminifu na kuondoa wasiwasi, na kutoa mchango wake katika kuhimiza usalama, utulivu na maendeleo kwenye eneo la Mashariki ya Kati.