Gazeti la Financial Times: kuizingira China si mkakati wa kudumu unaofaa
2023-04-06 21:57:17| cri

Gazeti la Financial Times la Uingereza limechapisha makala iliyoandikwa na Edward Luce akisema, China iko sahihi kwa kuona kwamba Marekani ndio inaizuia, kuizingira na kuishinikiza China, lakini ameonya kuwa kufanya hivyo si mkakati wa kudumu unaofaa.

Mwandishi huyu raia wa Marekani alisema sababu kadhaa zinazopelekea hali ya wasiwasi ya uhusiano kati ya China na Marekani ni kwamba Marekani haitaki kuacha nafasi yake ya kipekee inayofuatiliwa na nchi nyingine. Jaribio la rais Joe Biden kutaka kushirikiana na China liligonga mwamba baada ya Marekani kudungua puto la kuchunguza hali ya hewa la China. Alisema kwamba hatua kama hiyo ya kupita kiasi ilichochewa na makubaliano ya vyama viwili ambavyo vinachukulia mawasiliano yoyote na China kama ni udhaifu.

Alisisitiza kuwa Wamarekani wengi wanaona kuwa Marekani na China ziko katika vita baridi, lakini Marekani haiwezi kupata njia ya kushinda, kwa kuwa kuifanya China iweze kuitii si mkakati.

Alisema nchi inayojiamini kwa nguvu zake haipaswi kuogopa mazungumzo.