Kwa nini CPC yaanzisha mafunzo yenye maudhui maalum?
2023-04-06 13:55:14| cri

Hivi karibuni, Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imeitisha mkutano ikiamua kuanzisha mafunzo kuhusu utekelezaji wa Fikra ya rais Xi Jinping wa China kuhusu Ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya kwa wanachama na makada wote zaidi ya milioni 96 kuanzia mwezi Aprili mwaka huu. Je, mafunzo yenye maudhui maalum ni nini? Kwa nini CPC inaanzisha mafunzo kama hayo kwa wanachama wote? Mafunzo kama hayo yana umuhimu gani? 

Katibu wa Chama Mo Rongqing (wa tatu kutoka kushoto) akikagua masuala ya umaskini kwenye kijiji cha Jiabao, wilaya ya Antai, mji wa Liuzhou, mkoani Guangxi. 


Je, mafunzo yenye maudhui maalumu ya CPC ni nini?

Mafunzo yenye maudhui maalum ya CPC yanajumuisha elimu inayotolewa kwa njia tofauti na maudhui tofauti kwa wanachama wote. Katika nyakati na vipindi tofauti tangu kuanzishwa kwa CPC katika zaidi ya miaka 100 iliyopita, chama hicho kimeanzisha mafunzo mbalimbali kwa wanachama kwa kufuata mahitaji yake halisi. Wasomi wa utafiti wa CPC wanaona kuwa, moja ya siri za mafanikio ya CPC ambayo imeiongoza China kupata maendeleo na utulivu kwa pamoja ni kufanya vizuri katika kujifunza, na kutoa mafunzo ya maudhui maalum ni moja ya njia zenye ufanisi mkubwa za kuongoza sifa na uwezo wa makada wa chama hicho.


Kwa nini CPC inaanzisha mafunzo yenye maudhui maalum mwaka huu?

Vijana wakitoa huduma za kujitolea kwa wakazi mjini Beijing

Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, umeweka mipango kuhusu maendeleo ya China katika miaka mitano ijayo na muda mrefu zaidi, na kuweka Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye Umaalumu wa China katika Zama Mpya kwenye Katiba ya Chama cha CPC, na kuifanya iwe mwongozo wa utekelezaji wa hatua za CPC. Viongozi wa awamu mpya wa China wakiongozwa na Rais Xi Jinping, wanachukulia “kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu kubwa, na kulistawisha taifa la China” kuwa lengo la kimkakati la maendeleo ya uchumi na jamii ya China katika siku za baadaye. Rais Xi ameeleza kuwa, madhumuni ya kuanzisha mafunzo yenye maudhui mbalimbali ni “kuwaelekeza wanachama wote kukumbuka vizuri chama cha CPC ni nini, na majukumu ya CPC ni yapi, na kudumisha uhusiano wa karibu kati ya chama na wananchi.”


Mafunzo yenye maudhui maalum ya CPC yanaleta ushawishi gani?

 

Makada wa chama wanaofanya kazi vijijini

Kutokana na mafunzo matano yaliyofanyika tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, mafunzo hayo yamepata mafanikio mazuri. Kwa mfano, mwaka 2013 CPC ilianzisha mafunzo yenye maudhui ya kuwahamasisha wanachama kufanya kazi kwa kufuata hali halisi. Ili kushinda mapambano dhidi ya umaskini, CPC ilituma makatibu na makada zaidi ya milioni tatu katika vijiji maskini, ili kuwasaidia wanakijiji kuondokana na umaskini. Mwaka 2021, CPC ilifanikiwa kukamilisha lengo lake la kwanza la karne moja ambalo ni kutokomeza umaskini uliokithiri wakati wa Miaka 100 tangu kuanzishwa kwa chama hicho, na kujenga jamii yenye maisha bora katika pande zote.

Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC umeweka lengo wazi la kimkakati kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii, ambayo ni kutimiza kimsingi usasa wa kijamaa ifikapo mwaka 2035, na kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu ya kisasa ya kijamaa ifikapo katikati ya karne hii, ambalo ni “Lengo la Karne ya Pili”. Safari hii katika mafunzo yenye maudhui maalum, CPC inawataka wanachama wote kujifunza kwa kina na kuelewa Fikra ya Ujamaa wenye Umaalumu wa China katika Zama Mpya, wanachama na makada wa ngazi mbalimbali kufanya kikamilifu utafiti na ukaguzi katika ngazi ya shina ikiwemo vijiji, mitaa, viwanda, hospitali na shule, ili kuchunguza na kutatua matatizo. Kuzingatia kwa makini maendeleo yenye ubora wa juu ambayo ni jukumu kuu katika kujenga kwa pande zote nchi ya kisasa ya kijamaa, na kuwafanya wananchi wanufaike na matokeo halisi ya kutatuliwa kwa matatizo mbalimbali.