Mkuu wa UM awataka Taliban kufuta uamuzi wa kupiga marufuku wanawake wa Afghanistan kufanya kazi na UM
2023-04-06 09:06:40| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa mwito kwa Taliban kufuta uamuzi wao wa kupiga marufuku wanawake wa Afghanistan kufanya kazi na Umoja huo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema katibu mkuu wa umoja huo analaani vikali uamuzi huo wa Taliban, na kuutaja kuwa ni ukiukwaji wa haki za kimsingi za binadamu kwa wanawake. Amesema uamuzi huo pia umekiuka wajibu wa Afghanistan chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, na unakwenda kinyume na kanuni ya kutokuwa na ubaguzi, ambayo ni nguzo muhimu ya Katiba ya Umoja wa Mataifa.