Karakana ya Luban ya China yaingiza nguvu mpya kwa wahandisi vijana wa Tanzania
2023-04-06 10:53:21| CRI

Ni furaha iliyoje kuwa nawe tena msikilizaji katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Kipindi cha leo kitakuwa na ripoti inayohusu karakana ya Luban ya China inavyoingiza nguvu mpya kwa wahandisi vijana wa nchini Tanzania, lakini pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi yatakayohusu jinsi wakulima wa parachichi nchini Kenya wanavyofaidika na kilimo hicho baada ya kuanza kuuza bidhaa hiyo nchini China.