Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alaani vikali safari ya Tsai Ing-wen nchini Marekani
2023-04-06 09:06:07| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China leo amesema, hivi karibuni Marekani imemruhusu kiongozi wa eneo la Taiwan Tsai Ing-wen kwenda Marekani, na kukutana na spika wa Baraza la Wawakilishi la Bunge Kevin McCarthy ambaye ni kiongozi wa tatu wa serikali ya Marekani, pamoja na maofisa na wabunge wengine bila kujali upinzani na onyo la China, hatua ambayo imeweka jukwaa kwa Tsai Ing-wen kutoa kauli za ufarakanishaji.

Amesema lengo la hatua hiyo ni kufungua mawasiliano rasmi kati ya Marekani na Taiwan na kuinua uhusiano kati ya pande hizo mbili, kitendo ambacho kimekiuka vibaya Kanuni ya China Moja na Taarifa Tatu za Pamoja kati ya China na Marekani, kimekiuka vibaya mamlaka ya China na ukamilifu wa ardhi ya China, na kutoa ishara mbaya ya kimakosa kwa wafarakanishaji wa Taiwan. China inapinga na kulaani vikali kitendo hicho cha Marekani.