Kampuni ya Huawei ya China na washirika mbalimbali wakiwemo kampuni ya mawasiliano ya MTN ya Uganda na kampuni ya Saruji ya HIMA, hivi karibuni wametangaza mradi wa kujenga kiwanda cha kwanza cha saruji kinachotumia teknolojia ya 5G huko Kampala, Uganda.
Mradi huo unakuwa mradi wa kwanza wa kutumia teknolojia ya 5G kwa njia ya kibiashara kwenye sekta ya uzalishaji nchini Uganda. Mradi huo unalenga kuongeza ufanisi wa uzalishaji kiwandani kupitia matumizi ya teknolojia ya 5G ambayo inatarajiwa kuwezesha usambazaji wa data wa papo kwa hapo katika eneo la uzalishaji, ufuatiliaji wa mali na kadhalika.
Meneja mkuu wa kampuni ya Huawei nchini Uganda Bw. Gao Fei amesema Huawei itaendelea kushirikiana na pande husika ili kusaidia mageuzi ya kidigitiali katika sekta mbalimbali nchini Uganda.