China yapinga kithabiti safari ya Tsai Ing-wen nchini Marekani
2023-04-06 09:16:14| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China siku ya Alhamisi ametoa kauli kuhusu "safari ya kuunganisha" ya kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-wen kupitia Marekani.

Katika kauli hiyo, China imetoa misimamo yake kuhusu suala hili pamoja na mambo mengine mbalimbali. Baadhi ya misimamo hiyo ni kama ifuatayo:

Katika siku za hivi karibuni, kwa kutojali upingaji mkali na onyo za mara kwa mara zilizotolewa na China, Marekani imeruhusu kwa ukaidi "safari ya kuunganisha" ya Taiwan Tsai Ing-wen kupitia Marekani na mkutano wa hadhi ya juu kati ya Tsai na Spika wa Bunge la Marekani Kevin McCarthy, ambaye ni ofisa wa tatu wa ngazi ya juu zaidi wa Serikali ya Marekani. Pia imeruhusu maofisa wa Marekani na wajumbe wa bunge kuwasiliana na Tsai, na kutoa jukwaa kwa Tsai kutoa kauli za makundi ya kutaka Taiwan ijitenge na China.

Msemaji huyo amesema, kimsingi, Marekani inashirikiana na watawala wa Taiwan na kuratibu majaribio ya watu wanaotaka "Taiwan ijitenge na China" kwa kutekeleza shughuli za kisiasa katika ardhi ya Marekani, kushiriki katika mawasiliano rasmi kati ya Marekani na Taiwan, na kuinua uhusiano halisi kati ya Marekani na upande wa Taiwan.

Vitendo hivyo vimekiuka sana kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, vimekiuka kwa kiasi kikubwa mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya China, na kutoa ishara mbaya sana kwa vikundi vinavyotaka Tawain ijitenge na China."

China imeeleza kupinga na kulaani vikali vitendo hivyo.

Kauli hiyo imesisitiza kuutaka upande wa Marekani kufuata kikamilifu kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, kuchukua hatua kwa ahadi yake ya kutounga mkono "Taiwan kujitenga na China" au "China mbili" au "China moja, Taiwan moja," kusitisha mara moja aina zote za mawasiliano rasmi na Taiwan, kuacha kupandisha hadhi ya uhusiano halisi kati yake na Taiwan, kuacha kuleta mivutano kwenye Mlango-Bahari wa Taiwan, kuacha kutumia Taiwan kuizuia China, na kuacha kwenda chini zaidi kwenye njia mbaya na hatari.