Rais Xi afanya mazungumzo ya pande tatu na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen
2023-04-07 08:36:02| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana hapa Beijing alifanya mazungumzo ya pande tatu na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya Bibi Ursla von der Leyen.

Rais Xi amewaambia viongozi hao kuwa China na Umoja wa Ulaya zina maslahi mengi ya pamoja, ambayo yanazidi tofauti zilizopo kati ya pande hizo mbili. Rais Xi amesema kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili ni muhimu, na kukumbusha kuwa ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya haulengi upande wa tatu.

Bibi Von der Leyen amesema China na Umoja wa Ulaya ni washirika wakubwa wa kibiashara wa kila upande, na uchumi wa pande hizo mbili umefungamana sana, na kuyumbisha hali hiyo si chaguo kwa Umoja wa Ulaya.

Rais Macron amesema kwa sasa dunia ina changamoto nyingi, na kuwa China na Umoja wa Ulaya wanahitaji kuimarisha mawasiliano na kuheshimiana, uwazi na kuvumiliana.