Vikwazo dhidi ya mfarakanishaji mwenye msimamo mkali anayetaka ‘Taiwan ijitenge' vyatangazwa
2023-04-07 14:19:17| cri

Msemaji wa Ofisi ya Kazi ya Taiwan ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China leo ametangaza vikwazo zaidi dhidi ya mfarakanishaji mwenye msimamo mkali Bi-khim Hsiao anayetaka "Taiwan ijitenge", ikiwa ni pamoja na kumpiga marufuku yeye na jamaa zake kuingia China Bara, Hongkong na Macao, pia kuwazuia wafadhili wake na makampuni husika kushirikiana na mashirika na watu binafsi wa China Bara, na kuchukua hatua nyingine zote muhimu za adhabu, pamoja na uwajibikaji wa maisha yote kwa mujibu wa sheria.

Msemaji huyo pia alisema kuwa historia imethibitisha na itaendelea kuthibitisha kwamba "kujitenga kwa Taiwan" ni kosa, na  wanaotegemea nguvu za nje kuchochea kwa makusudi watashindwa. Amesisitiza kuwa mtu na nchi yoyote haipaswi kupuuza nia imara na nguvu kubwa ya China kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi.