Marais wa China na Ufaransa wafanya mazungumzo
2023-04-07 08:37:15| CRI

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ambaye yupo ziarani nchini China.

Kwenye mazungumzo hayo rais Xi ameeleza kuwa hivi sasa dunia inapata mabadiliko ya kihistoria, ambapo China na Ufaransa zikiwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zina uwezo na wajibu wa kushikilia uhusiano kati yao na kulinda amani, utulivu na ustawi duniani.

Rais Macron ameeleza kuwa Ufaransa inaipongeza China kwa kufuata kanuni za katiba ya Umoja wa Mataifa, kutoa mchango kwa ajili ya ufumbuzi wa masuala muhimu ya kimataifa, na inatarajia kuimarisha ushirikiano na China, ili kufanya juhudi za kutimiza amani na utulivu wa kudumu duniani.

Baada ya mazungumzo hayo viongozi hao wawili walishuhudia kutiwa saini kwa Makubaliano ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za kilimo, sayansi na teknolojia, usafiri wa anga, matumizi ya kiraia ya nishati ya nyuklia, maendeleo endelevu na utamaduni.