Chama cha wafanyabiashara na wanaviwanda cha Kenya, kimesema maonesho ya tatu ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika KNCCI yatakayofunguliwa huko Changsha, mkoani Hunan yatahimiza mauzo ya bidhaa za Kenya nchini China.
Naibu mwenyekiti wa kwanza wa chama cha KNCCI Bw. Eric Rutto, amesema mjini Nairobi kuwa maonesho hayo yatakuwa ya kwanza ambayo wafanyabiashara wa Afrika wanaweza kushiriki kwa njia ya ana kwa ana nchini China tangu mlipuko wa COVID-19 utokee.
Amesema maonesho hayo yatakuwa fursa nzuri kwa jumuiya ya biashara ya Afrika, kwa sababu yatawawezesha wafanyabiashara wa Afrika kuwasiliana na jumuiya ya uchumi ya China na kuendeleza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano unaonufaisha pande mbili.
Ameeleza Afrika itatumia shughuli hiyo itakayofanyika kutoka Juni 29 hadi Julai 2 kukusanya habari za soko kuhusu mahitaji ya wateja wa China.