Wataalamu wana wasiwasi juu ya kuongezeka kwa wagonjwa wa kifafa nchini Uganda
2023-04-07 22:19:51| cri

Wataalamu wa afya wameelezea wasiwasi wao kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kifafa nchini Uganda.

Kulingana na utafiti wa 2020-2022 uliofanywa na Kitivo cha Afya ya Umma cha Chuo Kikuu cha Makerere, kiwango cha maambukizi ya kifafa ni kikubwa kati ya wanawake ambao wanachukua asilimia 1.73 na asilimia 1.63 kwa wanaume.

Akizungumza kwenye mkutano wa kutolewa ripoti ya Utafiti wa Maambukizi ya Ugonjwa wa Kifafa Kitaifa na Majadiliano siku ya Jumatano mjini Kampala, mtafiti mkuu Prof Anthony Fuller alisema ugonjwa huo umesambaa kwa kiwango sawa kote nchini kuanzia karibu asilimia 0 hadi zaidi ya 5 katika wilaya maalum.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, eneo la mashariki lina kiwango cha maambukizi ya asilimia 2.16, likifuatiwa na eneo la kati na magharibi kwa asilimia 1.6 huku Kaskazini mwa Uganda kukiwa na idadi ndogo zaidi ya asilimia 1.35.