Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya mpira wa kikapu ya FIBA Africa
2023-04-07 22:20:29| cri

Tanzania imepewa nafasi ya kuandaa mashindano ya mpira wa kikapu barani Afrika kwa wanaume yanayojulikana kama FIBA AfroCan ambayo yanatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

Haya ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Mwenze Kabinda alipokuwa akihojiwa na gazeti la The Citizen.

Kabinda alisema mashindano hayo yamepangwa kufanyika kuanzia Mei 17 hadi 24, yakishirikisha nchi tisa zikiwemo Burundi, Eritrea, Ethiopia, Sudan Kusini, Somalia, Uganda, Rwanda, Sudan na wenyeji Tanzania.