Saudi Arabia na Iran zasaini makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kibalozi
2023-04-07 18:18:31| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang amesema China inaziunga mkono nchi za Mashariki ya Kati kujiamulia kimkakati, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kuzuia uingiliaji mambo ya ndani kutoka nje, na kushughulikia mustakabali wao wenyewe.

Qin alisema hayo alipokutana na mwenzake wa Saudi Arabia Mwanamfalme Faisal bin Farhan Al Saud na mwenzake wa Iran Hossein Amir-Abdollahian jana mjini Beijing. Baada ya mkutano huo Qin Gang alihudhuria hafla ya kusaini makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kibalozi kati ya Saudi Arabia na Iran.

Qin aliongeza kuwa China inakaribisha na kupongeza jitihada za Saudi Arabia na Iran katika kuboresha uhusiano kati ya nchi mbili. China inapenda kuendelea kufanya kazi ya uratibu, kuziunga mkono pande hizo mbili kujenga uaminifu na kuondoa wasiwasi, na kutoa mchango wake katika kuhimiza usalama, utulivu na maendeleo kwenye eneo la Mashariki ya Kati.

Saudi Arabia na Iran nazo zimepongeza kazi zilizofanywa na China kama nchi inayowajibika, pia kushukuru China kwa kuhimiza mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.