Rais Ebrahim Raisi wa Iran ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kushikamana kithabiti na kuwaunga mkono watu wa Palestina katika juhudi zao dhidi ya Israel.
Akizungumza kwa njia ya simu na rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Iran amesema nchi yake na Algeria zina msimamo wa pamoja kuhusu masuala mbalimbali ya kikanda na kimataifa, hususan suala la Palestina na utetezi wa haki za Wapalestina.
Rais Tebboune alisema anatarajia kuwa Palestina inaweza "kukombolewa" kutoka kwa Waisraeli kupitia ushirikiano wa nchi za Kiislamu.
Mazungumzo hayo yanafuatia mvutano katika eneo la mipaka kati ya Israel na Lebanon na eneo la Gaza kuongezeka wiki iliyopita ambapo wapiganaji kutoka kusini mwa Lebanon na Gaza walirusha makombora dhidi ya Israel, na Israel ikalipiza kisasi kwa mashambulizi ya anga.