Viongozi wote wa BRICS kuhudhuria Mkutano wa mwaka 2023 wa BRICS nchini Afrika Kusini
2023-04-10 08:57:11| cri

Mjumbe Maalum wa Afrika Kusini kwa Asia na BRICS Bw. Anil Sooklal amethibitisha kuwa, viongozi wote wa nchi za BRICS watahudhuria Mkutano wa Kilele wa kundi hilo utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Habari zinasema, maandalizi ya mkutano huo yanaendelea, na viongozi wa BRICS wamethibitisha kuhudhuria Mkutano huo, akiwemo rais wa Russia, Vladmir Putin.