Watu 44 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na watu waliokuwa na silaha katika vijiji viwili vilivyoko mkoa wa Sahel kaskazini mwa Burkina Faso.
Katika taarifa yake, Gavana wa eneo la Sahel Kanali Rodolphe Sorgho amesema, watu sita waliokuwa na silaha walishambulia vijiji hivyo viliyo karibu na tarafa ya Setenga usiku wa alhamis na ijumaa wiki iliyopita, na kusababisha majeruhi wengi na hasara za mali.
Kanali Sorgho amesema, vikosi vya usalama vimeanzisha mapambano dhidi ya wapiganaji hao na kufanya operesheni za kulinda amani kwenye eneo hilo.