Jengo la makazi huko Marseille nchini Ufaransa laporomoka
2023-04-10 22:03:42| cri

Jengo moja la makazi huko Marseille nchini Ufaransa liliporomoka jana alfajiri baada ya mlipuko kutokea na kusababisha watu wasiopungua watano kujeruhiwa na wengine wanane hawajulikani walipo.

Waendesha mashtaka wa Marseille walipozungumza na wanahabari wamesema jengo hilo lilikumbwa na mlipuko na kuwaka moto saa saba kasoro dakika 14 na baadaye likaanguka na kuathiri majengo mengine mawili ya karibu, na moja liliporomoka baada ya saa kadhaa.

Majengo hayo matatu yote si majengo yaliyo hatarini kuanguka. Kazi ya uokoaji na uchunguzi inaendelea huku wakazi 186 walioko karibu na majengo hayo wamehamishwa kwa sababu za kiusalama.