Iran yasema kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati yake na Saudi Arabia kutaleta manufaa katika ushirikiano wa kikanda
2023-04-11 08:36:43| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bw. Nasser Kanaani amesema, kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Iran na Saudi Arabia kutakuwa na manufaa makubwa katika ushirikiano wa kikanda, jambo ambalo litasaidia kupatikana amani, utulivu na usalama katika eneo hilo.

Bw. Kanaani pia amesema, makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia kuhusu kurejesha uhusiano wa kidiplomasia yamepata majibu chanya katika eneo hilo, na pia yamepongezwa katika ngazi ya kimataifa. Ameongeza kuwa, kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili pia kutakuwa na jukumu la kukuza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za kikanda, zikiwemo nchi hizo mbili.