Rais Xi Jinping afanya ziara ya ukaguzi mkoani Guangdong
2023-04-11 15:58:04| cri

Rais Xi Jinping wa China jana Jumatatu alifanya ziara ya ukaguzi katika mkoa wa kusini wa Guangdong.

Katika ziara yake mjini Zhanjiang, Rais Xi alitembelea kituo cha ufugaji wa samaki baharini, eneo la misitu ya mikoko, bandari na mradi wa ugawaji wa raslimali za maji.

Kwenye ziara hiyo Rais Xi alifahamishwa juhudi za kuendeleza sekta ya ufugaji wa samaki baharini, kuimarisha uhifadhi wa misitu ya mikoko, kuongeza muunganiko wa miundombinu ya uchukuzi, kusukuma mbele maendeleo ya pamoja ya mkoa wa Guangdong na mkoa jirani wa Hainan, na kuboresha ugawaji wa raslimali za maji.