Watu 6 wafariki katika ajali ya kuanguka kwa jengo la makazi mjini Marseille, Ufaransa
2023-04-11 10:01:48| cri


 

Watu 6 wamefariki baada ya jengo moja la makazi huko Marseille nchini Ufarasa kulipuka na kuwaka moto mapema Jumapili, ambapo liliangukia majengo mawili jirani.

Zaidi ya watu watano wamejeruhiwa, na wengine wanane hawajulikani walipo, huku watu 200 waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo wakihamishiwa sehemu salama.