Mamia ya wapalestina wajeruhiwa katika mapambano na askari wa Israel
2023-04-11 21:31:30| cri

Madaktari wa Palestina wamesema wapalestina zaidi ya 216 wamejeruhiwa katika mapambano na askari wa Israel kusini mashariki mwa mji wa ukingo wa magharibi wa Nablus.

Chama cha Msalaba Mwekundu cha Palestina kimetoa taarifa kuwa mapambano makali yametokea kati ya waandamanaji wanaopinga makazi ya wayahudi na askari wa Israel katika kijiji cha Beita, watu 22 wamejeruhiwa kwa risasi za mpira na wengine watu zaidi ya kumi wameathirwa na mabomu ya machozi yaliyorushwa na vikosi vya Israel.

Mapigano hayo yalitokea baada ya mawaziri 7 na wabunge 20 na wakazi zaidi ya 17,000 wa Israel kufanya maandamano kuelekea kwenye kituo cha “Avatar” kisichoidhinishwa kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi na kudai kukihahalisha.